Monday, January 26, 2015

WAKRISTU WAIJIA JUU SERIKALI WAKATAA MAHAKAMA YA KADHI

Dar es Salaam. Wakati macho na masikio ya Watanzania wengi yakielekea mjini Dodoma kesho katika vikao vya Bunge vinayotarajia kujadili Muswada wa Mabadiliko ya Sheria Mbalimbali, Jukwaa la Wakristo nchini limeitaka Serikali isitishe kujadili marekebisho ya Sheria ya Tamko la Sheria ya Kiislam ya mwaka 1964.
Taarifa iliyotolewa na Jukwaa hilo leo inasema Muswada huo unaolenga kuanzishwa kwa Mahakama ya Kadhi utasabisha kuvunjika kwa misingi ya Taifa hili kama lisilo la kibaguzi na kufungamana na dini yeyote.
Taarifa hiyo pia ilisema mapendekezo ya kurekebisha Sheria ya Tamko la Sheria za Kiislamu ni mapendekezo makubwa yatakayokuwa na athari kubwa na nzito; kwani yanahoji msingi wa dola ya Tanzania kama dola isiyokuwa ya kidini.

Dr SHEIN HANA MPINZANI CCM ZANZIBAR

Zanzibar. Kamati maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar imepitisha azimio la pamoja la kumtaka Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein kujitokeza kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya Urais uchaguzi unaotarajia kufanyika mwaka huu,imefahamika Visiwani humo.
Tamko hilo limetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Mohamed Aboud Mohamed alipokuwa akiwasilisha mada kuhusu mafanikio ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi katika Kongamano lililofanyika Ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Fidel Castro na kufunguliwa na Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein, huko Pemba.
Alisema kwamba maamuzi hayo yamelazimika kufanyika baada ya kufanyika tathimini na kuona Dk Shein ameonyesha mwelekeo mzuri wa kisiasa na kiuchumi katika kipindi cha uongozi wake kutokana na utekelezaji mzuri wa Ilani ya uchaguzi baada ya kushika wadhifa huo mwaka 2010.
“Kamati maalum ya Halmashauri Kuu Zanzibar tumepitisha makubaliano na kumuomba aongeze kipindi kingine cha kugombea Urais kwa sababu ametekeleza vizuri ilani ya uchaguzi,  sasa imebakia hiyari yake.”alisema Aboud ambaye  Mjumbe wa Halmashauri Kuu Taifa ya Cama hicho.
Aidha alisema kwamba katika kipindi chake Dk Shein ameonyesha uwezo, busara na hekima kubwa katika kuiongoza Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) na kufikia malengo ya kuanzishwa kwake ikiwemo kuondoa siasa za chuki na kujenga misingi ya umoja wa kitaifa kwa wananchi wake.
“Wakati ukifika tumekubaliana  katika Kamati Maalum Dk Shein achukuwe fomu ya kugombea nafasi ya Urais wa Zanzibar.”alisema Aboud na kuibua shangwe kwa washiriki wa Kongamano hilo.
Mwaka 2005  Makamo wa Rais Muungano Dk Mohamed Bilal alijitokeza kuchukua fomu na kuchuana na Rais mstaafu Amani Abeid Karume na kuibua hekaheka kubwa ya kisiasa kabla ya kuombwa kuondoa jina lake na wazee kwa madhumuni ya kulinda umoja katika kuelekea Uchaguzi Mkuu.

Thursday, January 22, 2015

WAFARANSA WAMUANGUKIA BIBI KIZEE ALIYETISHIA SERIKALI KUHUSU GESI MTWARA

Habari zalizotufikia, yule bibi kikongwe bi Somoe Issa, aliyeitishia serikali kutohamisha gasi ya Mtwara kuja Dar es Salaam, vinginevyo itageuka maji, amefuatwa na wafaransa wa kampuni ya Maurel et Prom kumuomba awafanyie tambiko la kuepusha madrill yao kuvunjika  mara kwa mara.

Kwa mujibu wa habari hizo, bibi huyo mwenye miaka 90, ambaye pia ni mkuu wa kaya katika kijiji cha msimbati,  ambako ndiko gesi inakotoka aliombwa kuwafanyia tambiko vigogo wa kampuni hiyo na wafanyakazi wao.

Taarifa hizo zinadai maabosi wa kampuni hiyo waliamuwa kumfuata baada ya kutonywa na mmoja wa wafanyakazi wao kuwa ni vyema wamuone bibi huyo, kwasababu walilalamikia uvunjikaji huo haukuwa wa kawaida. 

Bibi alikubali ombi lao na kufanya tambiko maalum la kuzuia mikosi na balaa na kuzuia mizimu kuvunja vifaa vya kazi

AVRIL FEAT OMMY DIMPOZ- KIBAO KINATAMBA SASA KENYA NA TANZANIA !

MISS TANZANIA MILLEN MAGESE AWA VIDEO MODEL !

KIJIWE CHA UGHAIBUNI !!Wednesday, January 21, 2015

MAJAMBAZI WAVAMIA KITUO NA KUUA POLISI WAWILI

Majambazi kadhaa wamevamilia kituo cha Polisi cha Ikwiriri kuuwa polisi wawili na kupora silaha usiku wa kuamkia leo.

Kwa mujibu wa habari hizo majambazi yalifanikiwa pia kuharibu gali la polisi zenye usajiri wa namba PT1965,marehemu hao ni koplo Edgar Milinga na Polisi konstebo Judith Timothy, na silaha zilizoibiwa ni SMG 2, Semi Riffle 3 na Anti Riot 1.Tunaendelea kufuatilia tukio hilo.
Mwili wa  marehemu Konstebo Judith Timothy 


Marehemu Judith Enzi za uhai wake

Tuesday, January 20, 2015

WAGOMBEA KUCHUKULIWA HATUA KWA KUSAMBAZA UZUSHI

MWIGULU APEWA CHOPA KUWANIA URAIS


Wakati Chama Cha Mapinduzi (CCM) kikiwa hakijaruhusu kampeni, Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba, ambaye amesema ameombwa na wazee na wasomi kuwania urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu, sasa atazunguka nchi nzima kwa kutumia helikopta kufanya mikutano ya hadhara kuzungumza na wananchi.

Hatua hiyo ya Mwigulu, ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM Tanzania Bara, ilitangazwa na Mwenyekiti wa Chama hicho Mkoa wa Geita, Joseph Msukuma jana.

Msukuma alisema ameamua kumpa Mwigulu helikopta yake ili aitumie kuzunguka nchini kote kutokana na kuwa mtetezi wa wananchi na maslahi ya taifa kwa jumla.

Alitangaza hatua hiyo katika mkutano wa hadhara ulioandaliwa na CCM Wilaya ya Morogoro mjini kwa ajili ya kuwashukuru wakazi wake kwa kuwachagua wagombea wa chama hicho katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliomalizika hivi karibuni.


CCM NEW YORK SPECIAL INVITATION KWENYE BASHHHHHHHHHHHHHHHH FEB 21